Joto la Moyo (Storymoja) – Hadithi ya Ndoto, Uvumilivu na Familia

Description
Joto la Moyo ni hadithi inayomhusu Bwire, mvulana anayeishi na nyanya na babu zake ambao hawana bee wala tee, ingawa wao ni wazazi wa daktari mashuhuri. Licha ya changamoto nyingi, Bwire ana ndoto kubwa maishani na amefanya vizuri katika mtihani wa taifa wa Darasa la Nane. Swali ni, atapataje pesa za kuendelea na shule ya upili? Je, ndoto yake itatekelezeka?
Nyanya yake, Bi Zahara, anamuambia Bwire hadithi za familia yao na changamoto waliopitia, huku taarifa anazopata kuhusu mama yake aliyeishi Eldoret zikimchochea kuanza safari kumtafuta. Hadithi hii inafundisha uvumilivu, ndoto, na mshikamano wa familia.
Author: Wafula Wa Wafula | ISBN: 9789966066619












