Kigogo (Storymoja) – Tamthilia ya Kiswahili FM3 & 4

Description
Tamthilia ya Kigogo ni tamthilia ya Kiswahili inayochambua baadhi ya masuala muhimu yanayoibuka katika nchi zinazoendelea za Afrika. Hadithi hii inaangazia maisha ya wakazi wa Sagamoyo wanapokuwa tayari kuadhimisha siku ya uhuru, huku wakijivunia maendeleo makuu. Hata hivyo, mgogoro unasababisha Soko la Chapakazi, tegemeo la wengi, kufungwa ghafla. Watoto na wakazi wanaulizwa: Je, viongozi walifunga soko kwa nia gani? Na wakazi wanaoilitegemea soko kujipa riziki watafanya nini?
Tamthilia hii inatoa picha halisi ya uhuru wa miaka mingi na kuchunguza: Je, uhuru huo unamfaidi nani? Ni tamthilia muhimu kwa wanafunzi wa Kiswahili, wasomaji wa tamthilia za kiadilifu, na wakazi wanaopenda kuangalia changamoto za kijamii.
ISBN: 9789966066633












