Mti wa Milele (Storymoja) – Hadithi ya Maadili Grade 3 & 4

Description
Mti wa Milele – Hadithi ya Kiswahili ya Kusisimua kwa Watoto wenye umri wa miaka 8-9 (Gredi 3 & 4) inayofundisha stadi muhimu za maisha. Kitabu hiki hufundisha uvumilivu, juhudi, na mbinu za kufanikisha malengo maishani kwa njia ya hadithi yenye kuvutia na yenye mafunzo.
Hadithi inamfuata Kobe, ambaye aliota ndoto ya mti unaozaa matunda ya kila aina. Je, mti huu upo kweli? Na ni siri gani itakayomsaidia kuupata? Hadithi hii ni chaguo bora kwa kujenga maadili mema, uvumilivu, na mshikamano kwa watoto.
ISBN: 9789966001726











