Mwongozo Kamilifu wa Wema Hauozi GD8 (Climax)

Description
Mwongozo huu umeandikwa kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi kuelewa tamthilia ya “Wema Hauozi” na kwa ujumla kumsaidia mwanafunzi kuelewa uchambuzi wa tamthilia yoyote ile. Mwandishi alizingatia vipengele ili kujenga ufahamu mpana wa mwanafunzi.
DHANA YA TAMTHILIA
Tamthilia ni kazi andishi ya fasihi inayowasilisha mchezo wa kuigiza. Tamthilia hutungwa kwa kuwahusisha wahusika wanaozungumziana moja kwa moja.










