KLB Top Scholar Kiswahili Grade 8

Description
KLB TopScholar Kiswahili Gredi ya Nane (Kitabu cha Mwanafunzi) ni kitabu cha Kiswahili kilichoidhinishwa na KICD na kinachotumika na Serikali ya Kenya katika shule za umma. Kimeundwa kikamilifu kulingana na Mtaala wa Kiumilisi wa Gredi ya Nane na kinawalenga wanafunzi wa Junior Secondary kukuza stadi zote nne za lugha: Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, pamoja na msingi madhubuti wa fasihi. Kitabu hiki kinatumia mbinu za kisasa za ujifunzaji na kinalenga kumwezesha mwanafunzi kukabiliana na maisha kwa ufasaha wa lugha ya Kiswahili.
Vipengele Muhimu na Faida:
-
Inafuata Mtaala wa Kiumilisi (CBC): Kimeandaliwa kikamilifu kulingana na Mtaala wa Kiumilisi wa Gredi ya 8 kutoka KICD.
-
Stadi Nne za Lugha na Fasihi: Kinashughulikia Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma, Kuandika, Sarufi na Fasihi kwa undani.
-
Mbinu Za Ujifunzaji Rahisi: Msamiati unafunzwa kimuktadha, na mazoezi ainati, mifano na picha zimetumika kumrahisishia mwanafunzi ujifunzaji.
-
Masuala Mtambuko na Umilisi: Kimelijumulisha masuala mtambuko ili kumkuza mwanafunzi mwenye umilisi, maadili na ujuzi wa kidijitali.
-
Ujifunzaji Unaovutia: Kimekuza upekee wa ujifunzaji kupitia sehemu kama Changamkia, Wazo Bainifu na Tafakuri, zilizolenga kumfanya mwanafunzi ashiriki kikamilifu na kujitathmini.
-
KIKD Approved na Serikali: Kimeidhinishwa na KICD na kinanunuliwa na Serikali ya Kenya kwa matumizi katika shule za umma, kuhakikisha ubora na uhalali wake.
-
Mazingira ya Kisasa: Kimelenga mazingira ya mwanafunzi na usasa ili kuhakikisha ujifunzaji unafanyika katika muktadha unaofaa.
Weka msingi imara wa Kiswahili kwa mwanafunzi wako wa Gredi ya 8. Nunua kitabu hiki chenye kuimarisha lugha kutoka Riki Bookshop leo!
ISBN: 9789966658944











