Laana ya Mkufu (Queenex)

Description
Mfalme Monamwezi hana muda mrefu wa kuishi. Anamrithisha ufalme mwanawe Kisangasanga. Mwanzoni, Kisangasanga anauendesha ufalme wa Watambele vyema hadi anapoenda kinyume cha maagizo ya baba yake. Ufalme unaanza kuporomoka. Mfalme Kisangasanga si mfalme wa wanadamu tena bali wa wanyama pangoni. Je, ataweza kurejea tena na kuendelea na uongozi? Laana ya Mkufu ni hadithi yenye ujumbe wa kipekee wa kumnasa msomaji yeyote anayeisoma.
David G. Maillu ni mwandishi tajika wa vitabu vya watoto. Anasifika kwa umiliki wake wa lugha na fasihi ya Kiswahili na kwa kuwachangamsha wasomaji kwa hadithi za kusisimua.
ISBN: 978-9966-075-50-5
9789966075505













