Longhorn Mwanga Wa Kiswahili Grade 7 (Rationalised)

Description
Longhorn Mwanga wa Kiswahili – Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 7 kimeandikwa kwa ustadi, umahiri mkubwa na kwa lugha ya kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya Saba. Kitabu hiki kinatosheleza kikamilifu mahitaji ya Mtaala wa Kiumilisi (CBC) pamoja na malengo ya elimu ya taifa la Kenya. Kimeshughulikia wanafunzi wote wakiwemo walio na mahitaji maalumu pamoja na wanaoishi kwenye mazingira mbalimbali. Kitabu hiki kitamwangazia na kumwezesha mwanafunzi kuwa na uwezo wa kuwasiliana na kushirikiana na wenzake, kuwa mwenye kuadilika, kujiamini na kujithamini, kuwaza kwa kina na kupata suluhu ya matatizo, kuwa raia mwadilifu na mzalendo, na kutumia vifaa mbalimbali vya kidijitali.
Upekee wa kitabu hiki ni kuwashirikisha wanafunzi kwa kiwango kikubwa katika ujifunzaji. Mzazi au mlezi pia ameshirikishwa hasa katika shughuli za ziada kwa njia rahisi ya kuelimisha na kuburudisha. Mwishoni mwa kila suala kuu kuna zoezi la marudio la kumchangamsha mwanafunzi ili kukumbuka aliyojifunza. Kitabu kina mwongozo wa mwalimu unaomwelekeza mwalimu katika kutekeleza wajibu wake, na majibu tarajiwa ya mazoezi yote pamoja na shughuli zote za ujifunzaji yametolewa. Kwa kuchanganua Msimbocode wa QR, wanafunzi wanaweza kupata Matini za Kidijitali za Video na Sauti zinazoboresha ujifunzaji. Waandishi wa kitabu hiki ni walimu na watahini wenye ujuzi wa kutosha katika ufundishaji na utahini wa somo la Kiswahili kwa miaka mingi.
-
Lugha Inayomfaa Mwanafunzi: Kimeandikwa kwa lugha ya kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya 7 kwa ustadi na umahiri mkubwa.
-
Ushirikishwaji wa Kina: Kinawashirikisha wanafunzi kwa kiwango kikubwa pamoja na wazazi na walezi kupitia shughuli za ziada za kuelimisha na kuburudisha.
-
Mahitaji Yote Yanashughulikiwa: Kinawashughulikia wanafunzi wote wakiwemo walio na mahitaji maalumu na wanaoishi kwenye mazingira mbalimbali.
-
Teknolojia ya Kisasa: Kina Msimbocode wa QR unaowapa wanafunzi Matini za Kidijitali za Video na Sauti kwa ujifunzaji shirikishi.
-
Ujuzi wa Kina: Kinakuza kuwasiliana, kushirikiana, kuadilika, kujiamini, kuwaza kwa kina, na utumiaji wa vifaa vya kidijitali.
Mwangaze mwanafunzi wako kwa maarifa ya Kiswahili angavu — Nunua nakala yako ya Longhorn Mwanga wa Kiswahili – Gredi ya 7 kutoka Riki Bookshop, duka la vitabu linaloaminika nchini Kenya kwa nyenzo bora za kielimu!
ISBN:Â 9789966643759












