Moran Stadi za Kiswahili Lugha Grade 3 (Rationalised)

Description
Moran Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya Tatu ni kitabu cha kiada kilichoandaliwa kwa ustadi kufuatana na Mtaala wa Kiumilisi. Kitabu hiki kinatumia Kiswahili cha kiwango cha mwanafunzi wa Gredi ya Tatu na kukuza umilisi wa lugha kupitia mbinu za kisasa na zinazomhusisha moja kwa moja mwanafunzi katika ujifunzaji wake.
Vipengele Muhimu vya Ujifunzaji:
-
Mtaala wa Kiumilisi:Â Kimeandaliwa kikamilifu kulingana na Mtaala wa Kiumilisi, kikishughulikia mada zote kuu na ndogo zilizomo na kufikia matokeo maalum yanayotarajiwa.
-
Maswali Dadidi:Â Kinatumia maswali dadidi kukuza ubunifu, uwazaji wa kina na umilisi wa utatuzi wa matatizo kwa wanafunzi.
-
Shughuli Mbalimbali:Â Kinajumuisha shughuli za kufanywa na mwanafunzi akiwa peke yake, na wenzake na katika vikundi kukuza ushirikiano na ujifunzaji wima.
-
Matumizi ya Lugha Sanifu:Â Kumwezesha mwanafunzi kutumia Kiswahili sanifu na kifaacho katika mazingira mbalimbali ya maisha ya kila siku.
-
Maadili na Masuala Mtambuko:Â Kinakuza maadili na kushughulikia masuala mtambuko kama ilivyoelekezwa katika mtaala, kukuza mwanafunzi anayestahili.
Kitabu hiki ni nyenzo bora kwa mwanafunzi wa Gredi ya Tatu kujenga stadi za kusikiliza na kuzungumza, kusoma, kuandika na sarufi kwa msingi imara.
ISBN:Â 9789966636010









